• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Kenya: Rais atia sahihi ugavi wa raslimali za kaunti

    (GMT+08:00) 2016-07-26 19:57:36
    Rais Uhuru Kenyatta ametia mswada wa ugavi wa raslimali kwa serikali za kaunti wa mwaka huu.

    Sheria hiyo itahakikisha ugavi sawa wa raslimali za kitaifa kati ya serikali za kaunti zote na kutoa nafasi kwa watu kutumia raslimali kwa biashara na uchumi.

    Pia inaweka kiwango cha pesa ambazo serikali za kaunty zinastahili kutumia kwa mishahara ya wafanyikazi wake na shughuli nyingine za serikali za kaunti hizo.

    Sheria hiyo inaorodhesha ruzuku zote ambazo serikali za kaunty zinapokea kutoka kwa serikali ya kitaifa.Pia inapendekeza hazina kuu iwe ikichapisha ripoti ya kila mwezi ya migao yote ya pesa inazotoa kwa serikali za kaunty.

    Kila hazina ya kaunty itahitajika kuonyesha pesa zote inazopokea kutoka kwa serikali kuu kwenye vitabu vyake vya hesabu za pesa.Mswada huo uliwasilishwa na spika wa bunge la senate Ekwe Ethuro kwa kiongozi wa taifa ili autie saini.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako