• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Waziri wa mambo ya nje wa Afrika Kusini kuongoza mkutano wa waratibu wa FOCAC

    (GMT+08:00) 2016-07-27 16:56:45

    Waziri wa mambo ya nje na ushirikiano wa kimataifa wa Afrika Kusini Maite Nkoana-Mashabane atashiriki na kuongoza mkutano wa waratibu wa Baraza la Ushirikiano wa China na Afrika FOCAC, uliopangwa kufanyika ijumaa wiki hii hapa Beijing.

    Bi. Nkoana-Mashabane atatumia fursa hiyo kuboresha uhusiano wa kisiasa na kiuchumi kati ya China na Afrika Kusini, nchi ambazo ni wenyeviti wenza wa FOCAC mpaka mwaka 2018.

    Mkutano wa waratibu utafanya tathmini ya maendeleo kwenye upande wa utekelezaji baada ya ahadi zilizotolewa katika mkutano wa FOCAC uliofanyika mjini Johannesburg, Afrika Kusini, Disemba mwaka jana. Mikutano hiyo inalenga kuimarisha mshikamano wa kihistoria wa urafiki kupitia ushirikiano wa kunufaishana ambao upo kati ya serikali na watu wa Afrika na China.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako