• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Rais wa China asisitiza umuhimu wa kuimarisha ulinzi wa nchi na kujenga jeshi la kisasa

    (GMT+08:00) 2016-07-27 19:41:15

    Rais Xi Jinping wa China amesisitiza kuwa kuimarisha ulinzi wa nchi na kuhimiza mageuzi ya jeshi ni hatua muhimu ya kusukuma mbele ujenzi wa jeshi la kisasa na kuongeza nguvu ya jeshi la China kwa kulingana na hadhi ya China kwenye jumuiya ya kimataifa na mahitaji ya kulinda usalama na maslahi ya taifa, ili kutoa uhakikisho imara kwa ajili ya kutimiza lengo la kustawisha tena taifa la China.

    Leo asubuhi rais Xi alikagua taasisi za Jeshi la ardhi la China, na kutoa salamu za Siku ya jeshi la China ambayo ni tarehe 1 Agosti, kwa wanajeshi wote wa Jeshi la Ukombozi la watu wa China.

    Hapo jana rais Xi Jinping pia alishiriki kwenye semina ya 34 ya ofisi ya siasa ya Kamati kuu ya chama cha kikomunisti cha China kuhusu kuimarisha ulinzi wa nchi na kuhimiza mageuzi ya jeshi.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako