• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Utumaji pesa kutoka Ulaya umeshuka kutokana na kujiondoa kwa Uingereza kwa Umoja wa Ulaya

    (GMT+08:00) 2016-07-27 19:58:02

    Fedha inayotumwa na wakenya wanaoishi Ulaya ilipungua kwa asilimia 6.3 mwezi uliopita hii ni kutokana na uamuzi wa Uingereza wa kujiondoa kwa Umoja wa Ulaya.

    Takwimu zilizotolewa jana na Benki Kuu inaonyesha kwamba fedha zinazotumwa kutoka Ulaya zimeshuka hadi sh bilioni 4.4 mwezi juni kutoka sh bilioni 4.7.

    Hata hivyo Jumla ya fedha iliyotumwa iliongezeka hadi sh bilioni 15.8 kutoka sh bilioni 14.8, mwezi mei.

    Kujiondoa kwa Uingereza katika Umoja Wa Ulaya mwezi uliopita, wachambuzi wanasema kutaathiri uchumi wa umoja wa ulaya na uchumi wa uingereza vibaya lakini kwa muda mfupi.

    Moja ya kampuni ya utumaji na upokeaji fedha kutoka nje, Dahabshiil, ilionya muda mfupi baada ya uingereza kujiondoa kwa umoja wa ulaya kwamba hatua hiyo uwenda ikaathiri fedha kutoka njena pia kuathiri uwekezaji katika kanda.

    Kiasi cha pesa kilichotumwa kutoka Amerika ya Kaskazini iliongezeka kwa asilimia 11.9 hadi sh bilioni 7.79 ambayo ilifikia asilimia 49.3 jumla ya mapato ya mwezi juni.

    mapato kutoka Ulaya ilifika asilimia 28 ikilinganishwa na asilimia 31 mwezi uliopita.

    Fedha zilizotumwa kutoka maeneo mengine ya dunia iliongezeka kwa asilimia 13 hadi sh milioni 3.6 na kufikia asilimia 22.8 ya jumla ya mapato yake.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako