• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Tamasha la kwanza la vijana wa Asia na Afrika lafunguliwa hapa Beijing

    (GMT+08:00) 2016-07-28 17:47:31

    Tamasha la awamu ya kwanza la vijana wa Asia na Afrika limefunguliwa leo hapa Beijing, na kuhudhuriwa na vijana 600 kutoka nchi 36 za mabara hayo mawili. Makamu wa rais wa China Bw. Li Yuanchao alipohutubia ufunguzi wa tamasha hilo, ameeleza matumaini yake kuwa vijana wa Asia na Afrika wataongeza uelewa wa jumuiya yenye hatma ya pamoja, kujitahidi kusukuma mbele mahusiano ya aina mpya ya kimataifa kwenye msingi wa ushirikiano wa kunufaishana, kulinda maslahi halali ya nchi zinazoendelea na kunufaisha watu wa Asia na Afrika. Fadhili Mpunji ana zaidi.

    Kwenye ufunguzi wa tamasha hilo, katibu wa kwanza wa sekritarieti ya kamati mkuu ya tawi la vijana la chama cha kikomunisti cha China Bw. Qin Yizhi amesoma barua ya pongezi kutoka kwa rais Xi Jinping wa China.

    "Moyo wa Bandung wa mshikamano, urafiki na ushirikiano uliothibitishwa kwa pamoja na viongozi wakongwe wa nchi za Asia na Afrika, umefanya kazi muhimu katika kuhimiza ushirikiano kati ya Asia na Afrika, na kuyaelekeza mahusiano ya kimataifa kwenye njia sahihi. Natumai kuwa vijana wa sasa wanaweza kurithi na kuenzi moyo wa Bandung, kuimarisha mawasiliano na kufundishana, kuzidisha maelewano, kusukuma mbele ushirikiano wa kunufaishana, na wajitolee kwa ajili ya kutimiza ndoto ya ustawi wa Asia na Afrika, kwa ajili ya kuhimiza maslahi ya watu wa Asia na Afrika, na vilevile kwa ajili ya amani na maendeleo ya binadamu wote!"

    Watu wa nchi za Asia na Afrika wamejenga urafiki tangu enzi na dahari. Uzoefu wa kihistoria unaofanana na malengo ya pamoja ya kutimiza maendeleo vimewafanya watu wa Asia na Afrika waungane mkono haswa katika wakati mgumu. Katika kipindi kipya cha kihistoria, kuimarisha ushirikiano kati ya Asia na Afrika bado kuna umuhimu mkubwa. Makamu wa rais wa China Bw. Li Yuanchao anasema,

    "Nchi za Asia na Afrika kuimarisha ushirikiano na kujikakamua, kutasaidia kuchochea uhai mpya katika mabara mawili ya Asia na Afrika, na pia kutasaidia kutatua matatizo na changamoto zinazowakabili binadamu wote kwa pamoja. Natumai kuwa vijana wa Asia na Afrika wataweza kujenga mtizamo wa jumuiya yenye hatma ya pamoja, kushirikiana na kufanya bidii kwa pamoja, ili kusukuma mbele ujenzi wa mahusiano ya kimataifa ya aina mpya kwenye msingi wa ushirikiano wa kunufaishana, kulinda vizuri zaidi maslahi halali ya nchi zinazoendelea na kunufaisha watu wa Asia na Afrika."

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako