• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Uwekezaji unakuwa injini mpya ya kukuza ushirikiano kati ya China na Afrika

    (GMT+08:00) 2016-07-30 20:27:24

    Waziri wa mambo ya nje ya China Wang Yi amesema China na Afrika zinatafuta mtindo mpya wa ushirikiano wa kunufaishana kati yao, na uwekezaji unakuwa injini mpya ya kuhimiza ushirikiano huo.

    Wang amesema hayo jana aliposhiriki kwenye mkutano wa kuratibu utekelezaji wa makubaliano yaliyofikiwa kwenye mkutano wa kilele wa Johannesburg wa Baraza la Ushirikiano Kati ya China na Afrika FOCAC. Mkutano huo wa kuratibu ulifanyika hapa Beijing na kuhudhuriwa na mawaziri zaidi ya 100 kutoka nchi za Afrika.

    Wang amesema makubaliano mbalimbali ya ushirikiano yamesainiwa kati ya China na Afrika kabla na baada ya mkutano huo, na mengi yao yanajikita kwenye sekta ya uwekezaji. Ameongeza kuwa ikilinganishwa na msaada, ushirikiano wa uwekezaji unaweza kuchangia maendeleo ya sekta ya viwanda barani Afrika na kuongeza uwezo wa kujiendeleza kwa nchi za Afrika, pia unasaidia kuuza mitambo, teknolojia na bidhaa za China kwa njia ya ushirikiano wa kiviwanda barani humo ili kukuza uchumi wa China.

    Habari pia zinasema, Bw. Wang jana hapa Beijing alikutana na wenzake wa nchi sita za Afrika waliokuja China kuhudhuria mkutano huo.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako