• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Mwani kwenye miti na miamba unaundwa na viumbe vitatu

    (GMT+08:00) 2016-08-02 09:39:25

    Mwani kwenye miti na miamba una hadhi muhimu katika biolojia.

    Mwanzoni wanasayansi waliuchukua kuwa mmea, lakini mwaka 1868, mwanasayansi wa Uswisi Simon Schwendener aligundua kuwa huu si mwani tu, bali ni mkusanyiko wa kuvu na mwani mdogomdogo. Baadaye wanasayansi wengine walithibitisha kuwa kuvu na mwani viliishi pamoja kwa kutegemeana. Mwani unazalisha lishe zinazohitajiwa na kuvu kwa mwanga wa jua, na kuvu inaupatia mwani madini, maji na ulinzi. Kabla ya hapo, watu hawakuwahi kutambua uhusiano wa kunufaishana kati ya viumbe mbili. Ili kueleza uhusiano huo, Wajerumani wawili, Albert Bernhard Frank na Heinrich Anton de Bary, walibuni neno jipya la "symbiosis" kwa maneno mawili ya Kigiriki, ambalo linamaanisha "kuishi pamoja".

    Katika miaka 150 baada ya Bw. Schwendener kugundua ukweli wa mwani kwenye miti na miamba, wanabiolojia walijitahidi kukuza mwani huo katika maabara na wote walishindwa.

    Hivi karibuni prof. Toby Spribille kutoka Chuo Kikuu cha Graz, Austria na wenzake walipopima RNA za mwani, waligundua aina mbili za kuvu. Halafu walipima aina 52 za mwani duniani, na kugundua kuwa zote ni mkusanyiko wa aina moja ya mwani na aina mbili za kuvu. Hii inamaanisha kwamba ni kawaida kwa mwani kuundwa na viumbe vitatu.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako