• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Kampuni ya China yaanza ujenzi wa mtandao wa kusafirisha umeme kati ya Ethiopia na Kenya

    (GMT+08:00) 2016-08-02 18:50:20

    Kampuni ya vifaa na teknolojia za umeme ya China CET, imeanza ujenzi wa nyaya za kusafirisha umeme wa voti kubwa kati ya Ethiopia na Kenya.

    Mradi huo ambao ujenzi wake unaanzia upande wa Ethiopia, na urefu wake ni zaidi ya kilometa elfu moja kwa upande wa Kenya na kilometa zaidi ya 400 kwa upande wa Ethiopia, una thamani ya dola bilioni 1.26 ambazo zimetolewa na Benki ya Maendeleo ya Afrika AfDB.

    Akitangaza kuanza kwa ujenzi huo ofisa wa shirika la umeme la Ethiopia anayeshughulikia miradi Bw Reta Nigussie, amesema mradi huo utakapokamilika utakuwa chanzo kizuri kwa fedha za kigeni kwa Ethiopia, kwa kuwa itaiuzia Kenya na nchi nyingine za Afrika Mashariki MW 2000.

    Bw Reta amesema ana matumaini kuwa mradi huo utakamilika kama ilivyopangwa, kwa kuwa kampuni ya China inayojenga mradi huo imekamilisha mradi mwingine wa umeme nchini Ethiopia.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako