• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Tunaweza kupunguza joto nyumbani kwa viyoyozi, lakini tunawezaje kupunguza joto mijini?

    (GMT+08:00) 2016-08-03 11:17:19

    Miji imerahisisha maisha yetu, lakini pia inasumbuliwa na joto kali katika majira ya joto. Kwa mfano, joto mjini Beijing ni kubwa zaidi kuliko vijijini kwa nyuzi 3.3 sentigredi, na joto la ardhini ni kubwa zaidi kuliko vijijini kwa nyuzi 20!

    Joto kali linatokana na sababu zifuatazo:

    1. Kuna miti michache zaidi mijini kuliko vijijini. Miti inaongeza unyevu hewani, na kuvukizwa kwa unyevu kunasaidia kupunguza joto.

    2. Saruji na lami zinaweza kuhifadhi joto jingi la jua.

    3. Mwanga wa jua unarudishwa kati ya majengo mbalimbali na kusababisha ongezeko la joto.

    4. Majengo marefu wa mijini yanazuia upepo.

    5. Magari, mashine za viwandani, vyombo vya umeme vya nyumbani na na idadi kubwa ya watu vinasababisha joto jingi.

    Kutokana na sababu hizi, joto la mijini na vijijini lina tofauti kubwa zaidi baada ya jua kutua. Ukiwa kijijini wakati wa jioni utahisi baridi ya kupendeza, lakini mjini utahisi majengo yote yanaendelea kutoa joto jingi.

    Hivi sasa wajenzi wa miji wamechukua hatua mbalimbali ili kutatua tatizo hili, zikiwemo kuongeza maeneo ya miti na mito mijini, kupaka majengo kwa rangi zisizokoza ili kuzuia majengo yasihifadhi joto jingi, kupanga sehemu zisizo na majengo marefu mijini ili kuongeza upepo, na kubana matumizi ya nishati.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako