• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Kenya yanufaika katika biashara ya viwanda vya nguo ikishirikiana na China

    (GMT+08:00) 2016-08-04 18:45:20

    China na Kenya zinaendelea kunufaika na Dira ya maendeleo ya Kenya kuelekea mwaka 2030, kupitia ushirikiano kwenye sekta ya nguo.

    Akiongea mjini Mombasa kwenye kongomano la siku mbili kati ya China na Afrika kuhusu sekta ya nguo, makamu mkuu wa Chuo Kikuu cha Moi Profesa Richard Mibey, akitolea mfano ruwaza ya Kenya kuelekea mwaka 2030 amesema uuzaji nje wa pamba kutoka Afrika unachangia asilimia 13 ya soko la pamba duniani, wakati China ni nchi inayoongoza duniani kwa mauzo ya nyuzi za pamba. Hali hiyo inaifanya China na Bara la Afrika kuwa wahusika wakuu katika biashara hiyo.

    Profesa Mibey amesema Chuo Kikuu cha Moi ambacho ni miongoni mwa vyuo vinavyoongoza kwenye tafiti barani Afrika, kimeitambua sekta ya pamba, kama itashirikisha wadau wengine, inaweza kuleta maendeleo ya kudumu nchini Kenya na kwingineko Barani Afrika.

    Makamu mkuu wa Chuo Kikuu cha Donghua cha China Bw. Cui Yunhua amesema, chuo chake na Chuo Kikuu cha Moi, wameandaa mkutano huo kutokana na ushirikiano wao wa muda mrefu kwenye sekta ya nguo.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako