• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Kenya na China zatoa mafunzo ya usimamizi wa reli ya mwendo kasi

    (GMT+08:00) 2016-08-05 09:44:05

    Serikali ya Kenya imewekeza mradi mkubwa wa mafunzo kuhusu usimamizi wa reli ya kasi SGR inayojengwa na China mara utakapokabidhiwa mwezi Juni mwaka ujao.

    Katibu mkuu katika wizara ya uchukuzi Irungu Nyakera amesema serikali imetoa kipaumbele kwa kuwa na watu wengi wenye utaalam wa kuendesha reli hiyo ya kisasa.

    Reli hiyo inajengwa na kampuni ya China CRBC kuunganisha mji wa Nairobi na Mombasa, ina urefu wa kilomita 472, na mpaka sasa, Wakenya karibu elfu 30 wameajiriwa kufanya kazi katika idara mbalimbali za mradi huo.

    Nyakera amesema ushirikiano uliojengwa kati ya serikali ya Kenya na CRBC umesaidia kuhamisha ufundi kutoka wahandisi wa China hadi mafundi wa Kenya wanaofanya kazi katika mradi huo.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako