• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Shimo la baharini lenye kina kirefu zaidi duniani lagunduliwa huko Sansha China

    (GMT+08:00) 2016-08-05 10:51:25

    Shimo la baharini lenye kina kirefu zaidi duniani limegunduliwa katika kisiwa cha matumbawe cha Yongle huko Sansha, China. Shimo hilo lina kina cha mita 300.89.

    Mashimo ya rangi ya buluu baharini ni mandhari zisizoonekana mara kwa mara duniani. Kabla ya hapo, mashimo yenye kina kirefu zaidi duniani ni pamoja na shimo la Dean's nchini Bahamas lenye kina cha mita 202, shimo la Dahab nchini Misri lenye mita 130, shimo la Belize nchini Honduras lenye mita 123 na shimo la Gozo nchini Malta lenye mita 60.

    Baada ya kufanya uchunguzi, watafiti wamegundua kuwa shimo hili linaelekea chini hadi mita 160, halafu linaelekea upande wa kaskazini. Zaidi ya aina 20 za samaki wanaishi katika shimo la Yongle wakiwemo taa wa porcupine, snailfish na parrot fish. Watafiti pia wamegundua kuwa shimo hili haliunganishwi na bahari nje yake, na maji chini ya mita 110 kimsingi hayana hewa ya oxygen.

    Mtaalamu wa kamati ya uhifadhi wa mazingira ya kiviumbe ya mji wa Sansha Bw. Gai Guangsheng alipopiga mbizi katika shimo hili, aliona kiumbe kisichotambuliwa cha baharini chenye urefu wa mita 2 hivi ambacho kinafanana na kamba, na kuna nyuzi nyingi zinazofanana na maporomoko juu ya miamba ndani ya shimo hili.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako