• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Tyson Fury, afunguliwa mashtaka kwa kutumia dawa za kuongeza nguvu

    (GMT+08:00) 2016-08-05 15:02:52

    Bingwa wa dunia uzito wa juu Tyson Fury, amefunguliwa mashtaka ya kutumia dawa zilizopigwa marufuku michezoni, na chama cha kupambana na dawa hizo Uingereza, Ukad. Ukad, ilimsimamisha Fury Juni 24 mwaka huu, siku ambayo Bondia huyo alitangaza kufuta pambano lake la marudiano na Wladimir Klitschko kwa sababu ya majeruhi, lakini Fury alikata rufaa na hukumu hiyo ikaondolewa.

    Ukad imesema imemfungulia tena mashtaka Fury na binamu yake Hughie Fury, kufuatia maneno yao kwenye ukurasa wao wa Twitter na hatma yao, itaamuliwa kwenye jopo la taasisi ya taifa ya kupambana na kuzuia, utumiaji dawa zilizopigwa marufuku michezoni, (NADP).

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako