• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Mkutano wa Baraza la ujasiriamali kwa vijana wa China na Afrika wafanyika Guangzhou, China

    (GMT+08:00) 2016-08-08 17:40:38

    Mkutano wa Baraza la ujasiriamali kwa vijana wa China na Afrika umefanyika hivi karibuni mjini Guangzhou, China. Katika mkutano huo, wajumbe vijana wa China na Afrika wamebadilishana uzoefu wa ujasiriamali na kubadilishana maoni kuhusu masuala wanayoyafuatilia kwa pamoja, shughuli ambazo zimezidisha mawasiliano na maelewano kati ya wajasiriamali vijana wa pande hizo mbili.

    David Kandi ni kijana kutoka Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo aliyeanzisha biashara yake kwenye mtandao wa Internet. Amesema alianza shughuli zake kutokana na wazo la kuwasaidia wanafunzi waliorudi nyumbani baada ya kumaliza masomo nje ya nchi kupata ajira.

    "Nilikuwa nafikiria namna ya kutumia ujuzi wa kompyuta waliojifunza kuwasaidia kupata ajira. Kwa vipi tunaweza kuanzisha shughuli zetu? Nilifikiria kwamba bado kuna upungufu nchini kwetu katika sekta ya teknolojia ya mawasiliano ya habari, na watu hupendelea kujifunza ujuzi wa eneo hili nje ya nchi, kwa nini tusianzishe taasisi ya mafunzo moja kwa moja katika nchi yetu ili kutoa mafunzo kwa watu wanaohitaji teknolojia hizi?"

    Mwanzo kawaida ni mgumu. Kandi amesema, ili kuweza kutambuliwa kwenye soko, timu yake iliwahi kutoa mafunzo bila malipo kwa wateja. Hatimaye, taasisi waliyoanzisha ilikua kutoka wanafunzi 50 tu, hadi kuwa kampuni kubwa inayoshughulika na usanifu wa tovuti na software na huduma za ujasiriamali nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo.

    Hivi sasa mabadiliko makubwa ya kiuchumi na kijamii yanatokea katika nchi mbalimbali duniani, huku teknolojia mpya, sekta mpya na mitindo mipya vikiendelea kubuniwa, hali inayotoa fursa nyingi kwa wajasiriamali vijana. Katika Afrika ya leo, ujasiriamali wa vijana umekuwa si jambo geni, na wakati huohuo changamoto zinazowakabili pia si ndogo.

    Ingawa nchi na sehemu tofauti zina mazingira tofauti kwa ujasiriamali, lakini changamoto zinazowakabili wajasiriamali vijana zote zinafanana. David Kandi anaona kuwa, uungaji mkono wa serikali ni muhimu kwa wajasiriamali vijana.

    "linalonivutia zaidi kwenye baraza hilo ni kwamba serikali na taasisi za China zinaunga mkono sana wajasriamali vijana, ikiwemo misaada iliyotolewa na Shirikisho la wanawake kwa wajasiriamali wanawake. Ukiwa kijana, ni jambo zuri kwa vipaji vyako kugunduliwa na kutambuliwa. Kama nchi za Afrika zikiweza kutoa huduma kama hizi kwa vijana, bila shaka itasaidia sana maendeleo ya ujasriamali wa vijana."

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako