• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Mradi wa ujenzi wa reli kukuza uchumi nchini Kenya

    (GMT+08:00) 2016-08-09 09:00:42
    Waziri wa miundo mbinu na Usafiri James Macharia amesema reli ya kasi ya wastan ambayo inajengwa na Kampuni ya China, itasaidia kukuza uchumi wa Kenya kwa kupunguza gharama za usafiri na kuboresha usafirishaji wa watu na bidhaa.

    Akiongea kwenye mkutano wa kilele wa miundombinu mjini Nairobi, Macharia amesema, mradi huo uliogharimu dola za Marekani bilioni 3.6 ambao hadi sasa umekamilika kwa asilimia 88, umeshachangia asilimia 2 ya ukuaji wa pato la taifa la nchi hiyo GDP.

    Macharia ameongeza kuwa, zaidi ya Wakenya 27,000 wameajiriwa chini ya mradi huo, huku miji ambayo reli hiyo inapita ikinufaika kwa kustawi biashara zao. Mbali na hayo amesema mradi huo umeongeza ufanisi wa Bandari ya Mombasa kwa kuwa unahakikisha mizigo inasafirishwa haraka kuliko njia ya usafiri wa barabara.

    Mradi huo unaofadhiliwa na Benki ya Exim ya China unatarajiwa kukamilika mwakani.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako