• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Teknolojia ya kurekebisha jeni za binadamu

    (GMT+08:00) 2016-08-09 16:24:18

    Hivi karibuni baadhi ya wanasayansi wametangaza kuwa mwaka huu watakusanya dola za kimarekani milioni 100 ili kuanzisha mpango wa kurekebisha jeni za binadamu.

    DNA ni molekuli kubwa ndani ya seli za viumbe ambayo umbo lake linafanana na ngazi mbili zilizounganishwa pamoja na kupindwa kama skurubu. DNA inabeba habari zote za urithi wa kiumbe, na kwenye DNA ziko jeni mbalimbali ambazo zinaamua tabia mbalimbali.

    Katika miaka ya hivi karibuni wanasayansi wamevumbua teknolojia mpya ya kurekebisha jeni za binadamu ambayo ni pamoja na hatua za kukata DNA, kuirekebisha na kuiunganisha tena. Kutokana na hatua ya kukata DNA, teknolojia hii pia imesifiwa kuwa mkasi wa jeni.

    Kwa nadharia, teknolojia hii itatumiwa kuondoa jeni mbaya za mimba ambazo zinasababisha ulemavu au magonjwa, lakini watu pia wana wasiwasi kwamba teknolojia hii huenda ikasababisha suala la kimaadili, ambalo baadhi ya watu wanaweza kurekebisha ovyo jeni za mimba.

    Mwishoni mwa mwaka jana, wanasayansi na wataalamu wa maadili kutoka nchi mbalimbali walifanya mkutano wa marekebisho ya jeni za binadamu huko Washington Marekani, na kuamua kwamba teknolojia hii inaweza kutumiwa kutibu magonjwa ya binadamu, lakini haiwezi kutumiwa kuzalisha watoto mchanga wasio na kasoro yoyote.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako