• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Mkutano wa kwanza wa baraza la diplomasia ya umma kati ya China na Afrika wafanyika

    (GMT+08:00) 2016-08-10 10:20:38

    Mkutano wa kwanza wa baraza la diplomaisia ya umma kati ya China na Afrika umefunguliwa jana huko Dar es Salaam, Tanzania.

    Baraza hilo linalenga kutekeleza uamuzi husika uliofikiwa katika mkutano wa kilele wa Johannesburg wa baraza la ushirikiano kati ya China na Afrika, na kuhimiza ushirikiano kati ya pande hizo mbili kuendelea kwa kina na upana.

    Akizungumza kwenye ufunguzi wa mkutano huo, Mkurugenzi wa shirikisho la diplomasia ya umma la China Bw. Li Zhaoxing amesema China na Afrika ni nguvu muhimu ya kuhimiza dunia kuendelea kwa mwelekeo wa haki na usawa.

    Serikali ya Tanzania kupitia Waziri wa Habari, Utamaduni na Michezo Bw. Nape Nnauye imepongeza juhudi za serikali ya China za kuisaidia nchi hiyo na Afrika kwa jumla. Amesema China na Afrika zimeshirikiana katika mambo mengi, ambapo China na Afrika zinabadilishana uzoefu wa kuboresha mawasiliano, na pia jinsi China inavyohusisha dunia katika suala la mawasiliano. Amesema anatumai mkutano huo utainufaisha Tanzania kuhusu namna ya kuboresha uhusiano wa nchi hiyo na Afrika kwa ujumla na China, na namna ya kuboresha utendaji kazi wa vyombo vya habari katika bara hilo.

    Naye mkuu wa mkoa wa Dar Es Salaam Paul Makonda, amepokea msaada wa shilingi milioni 45 pamoja na vifaa vingine vya kusaidia elimu katika mkoa huo. Amesema uwekezaji huo unatoa fursa ya ajira, na pia unaleta teknolojia mpya ambayo itasaidia upatikanaji wa habari zenye ubora zaidi.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako