• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Yanga yaipiga MO Bejaia 1-0

    (GMT+08:00) 2016-08-15 09:13:34

    Klabu ya Yanga ya Dar es Salaam imefufua matumaini ya kutinga hatua ya nusu fainali ya kombe la Shirikisho barani Afrika baada ya kuichapa MO Bejaia ya Algeria.

    Yanga imepata ushindi wake wa kwanza katika hatua ya makundi ya michuano hiyo leo kwa ushindi wa bao 1-0 na kujipatia point 3 muhimu.

    Bao la Yanga limefungwa mapema kabisa kunako dakika ya pili ya mchezo kupitia kwa Mrundi Amis Tambwe.

    Ushindi huu unaifanya Yanga kufikisha point 4 katika nafasi ya 4 ya kundi A, ikiwa bado iko nyuma ya MO Bejaia yenye point 5 sawa na Medeama ya Ghana, huku TP Mazembe ikiongoza kundi hilo kwa point 10

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako