• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Bonde lenye majimaji lagunduliwa kwenye satilaiti ya Titan ya Zohali

    (GMT+08:00) 2016-08-15 11:13:12

    NASA imetangaza ugunduzi mpya wa chombo cha uchunguzi cha Cassini kwamba kuna bonde kubwa lenye majimaji ya Methane kwenye satilaiti ya Titan ya sayari ya Zohali.

    Titan ni satilaiti pekee yenye hewa nzito katika mfumo wa jua, ambayo kimsingi ni hewa ya Nitrogen. Juu ya satilaiti hii kuna bahari na maziwa yenye majimaji ya Methane. Katika miaka kadhaa iliyopita chombo cha uchunguzi cha Cassini kilipopita kwenye satilaiti hii, kiligundua kuwa bahari ya Ligeia iliyoko katika ncha ya kaskazini inaungana na mabonde kadhaa meusi yanayofanana na utando wa buibui.

    Lakini wanasayansi hawakujua vitu ndani ya mabonde hayo kuwa ni majimaji au barafu. Mwaka 2013 chombo cha uchunguzi cha Cassini kilipopita tena Titan, kilichunguza mabonde hayo kwa makini. Uchambuzi mpya unaonesha kuwa chini ya mabonde hayo kuna kitu laini kinachong'ara, hivyo inakadiriwa kuwa ni majimaji ya Methane.

    Mabonde hayo membamba yana upana usiozidi kilomita 1, lakini yana kina kirefu, ambacho ni kati ya mita 240 hadi 570.

    Watafiti wanaona kuwa kuundwa kwa mabonde hayo huenda ni matokeo ya kuinuka kwa ardhi na mabadiliko ya usawa wa bahari, lakini bado hawajajua nguvu hizi mbili zilitoa mchango gani.

    Utafiti huo umetolewa kwenye gazeti la mawasiliano ya fizikia ya dunia la Marekani.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako