• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • China imerusha satilaiti ya kwanza ya majaribio ya quantum duniani

    (GMT+08:00) 2016-08-17 11:01:47

    China imerusha satilaiti ya kwanza ya majaribio ya quantum duniani katika kituo cha kurushia satilaiti huko Jiuquan China.

    Satilaiti hii imepewa jina na Mozi ambaye ni mwanafilosofia wa kale wa China.

    Je, quantum ni nini? Ina tabia gani za ajabu?

    Vitu vyote ulimwenguni viliundwa na vitu vidogovidogo, na quantum ndiyo ni vitu vidogovidogo vinaunda uzito, ukubwa na nishati ya vitu. Mwanafikizia wa Ujerumani Max Planck alitoa nadharia ya quantum mwaka 1900.

    Quantum ina tabia za ajabu. Tabia ya kwanza inaitwa "quantum superposition", yaani inaweza kuwa na hali nyingi kwa wakati mmoja. Sifa hii ikitumiwa, inaweza kuinua uwezo wa kompyuta zetu kwa kiasi kikubwa sana. Swali linalohitaji kuhesabiwa kwa miaka milioni 1.5 kwa kutumia kompyuta ya sasa, likihesabiwa na teknolojia ya quantum, litamalizika kwa sekunde moja tu.

    Tabia nyingine ya quantum inaitwa "quantum entanglement". Inamaanisha kuwa quantum mbili zinazofanana zikiwekwa pamoja zitakuwa na hali sawasawa, na ukizitengaisha tena, zitaendelea kuwa na hali sawasawa kama mapacha ambao mmoja anaweza kuhisi hisia ya mwingine akiwa mbali.

    Quantum pia ina sifa ya kutotengwa na kutonakiliwa. Sifa hii itatusaidia kuendeleza teknolojia ya upashanaji habari yenye usalama zaidi.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako