• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Yanga yaaga Kombe la Shirikisho kwa kipigo

    (GMT+08:00) 2016-08-24 10:04:51

    Timu ya Yanga ya Dar es Salaam imeaga mashindano ya kombe la shirikisho kwa kipigo cha mabao 3-1 kutoka kwa TP Mazembe ya DRC.

    Mechi hiyo ya marudiano ya Kundi A ambayo imepigwa mjini Lubumbashi nchini DRC, ilikuwa na umuhimu wa kuweka heshima kwa Yanga kwa kumaliza ikiwa na point 7 jambo ambalo limeshindikana.

    Katika mchezo mwingine, Medeama ya Ghana imekubali kipigo cha bao 1-0 kutoka kwa MO Bejaia nchini Algeria, na kufanya msimamo wa kundi A ubadilike, hali iliyopelekea Medeama kuungana na Yanga kufungasha virago.

    Msimamo wa kundi hilo unaonesha kuwa TP Mazembe ndiyo vinara wakiwa na point 13 wakifuatiwa na MO Bejaia yenye point 8 ikilingana na Medema yenye point 8 pia, huku wakilingana tofauti ya mabao ya kufunga na kufungwa, na Yanga inakamata mkia ikiwa na point 4.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako