• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Maonyesho ya 23 ya vitabu ya kimataifa yafunguliwa Beijing

    (GMT+08:00) 2016-08-25 21:16:14

    Maonyesho ya 23 ya vitabu ya kimataifa yanafunguliwa leo Beijing, China, nchi 16 za Ulaya ya Kati na Mashariki zikiwa ni wageni wa heshima zinashiriki kwa mara ya kwanza katika historia ya maonyesho hayo.

    Makampuni 2,400 kutoka nchi 86 yanashiriki kwenye maonyesho hayo yatakayofanyika hadi tarehe 28 mwezi huu.

    Naibu mkuu wa Idara ya habari, uchapishaji, Redio, Filamu na Televisheni ya China Bw. Yan Xiaohong amesema, ushiriki wa nchi 16 za Ulaya ya Kati na Mashariki zikiwa wageni wa heshima kwenye maonesho hayo unaweza kuhimiza mawasiliano na ushirikiano wa kiutamaduni kati ya China na nchi za Ulaya ya Kati na Mashariki.

    Naye Naibu waziri wa mambo ya nje na biashara wa Hungary Bw Istvan Ijgyarto amesema maonyesho hayo yanasaidia kuhimiza nchi za Ulaya ya Kati na Mashariki na China kuelewana na kuaminiana.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako