• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Kobe Bryant atunukiwa tuzo ya heshima

    (GMT+08:00) 2016-08-26 09:37:31

    Mkongwe wa mchezo wa mpira wa kikapu nchini Marekani NBA, Kobe Bryant, ametunukiwa tuzo ya heshima, na Meya wa mji wa Los Angeles, Eric Garcetti, kwa kuuwakilisha vyema mji huo, katika kipindi cha miaka 20 ya kucheza kikapu.

    Baada ya kupewa tuzo hiyo, familia ya Bryant, ilijumuika na wanasiasa wa mji wa Los Angeles, na kumfanyia sherehe ya kumpongeza kwa kutimiza umri wa miaka 38.

    Bryant alistaafu kucheza mpira wa kikapu mwezi April mwaka huu, baada ya kuandamwa na majeruhi ya muda mrefu, lakini akiweka historia ya kuwa mfungaji wa muda wote wa L.A Lakers, na kuisaidia Marekani kushinda medali ya dhahabu kwenye Olimpiki ya 2008, ya hapa Beijing, na 2012 London.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako