• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Katibu mkuu wa UN apongeza China kwa kuongeza ujumuishi wa mkutano wa G20

    (GMT+08:00) 2016-08-27 18:07:03
    Katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa Bw. Ban Ki-moon ameipongeza China kwa kufanya juhudi za kuongeza ujumuishi wa mkutano wa kilele cha kundi la G20.

    Bw. Ban amesema China ikiwa nchi mwenyekiti wa zamu wa kundi la G20 imewaalika viongozi wakuu wa nchi nyingi zinazoendelea kushiriki kwenye mkutano huo, zikiwemo nchi mwenyekiti wa Jumuiya ya ASEAN, Laos na nchi mwenyekiti wa Umoja wa Afrika Chad, na kufanya mkutano wa kilele wa safari hii kuwa unaohudhuriwa kwa wingi zaidi na nchi zinazoendelea katika historia ya kundi la G20.

    Bw. Ban amesema, wakati dunia inaendelea kukabiliwa na ufufukaji dhaifu wa uchumi, mkutano huo utakaofanyika mjini Hangzhou, mashariki mwa China unatakiwa kujadili njia ya kukabiliana na matatizo ya kiuchumi na masuala mengine kuhusu usimamizi duniani, na Umoja wa Mataifa utashiriki kwenye majadiliano hayo.

    Bw. Ban ameongeza kuwa China itaweka ajenda za maendeleo endelevu na mabadiliko ya hali ya hewa ili zijadiliwe kwa pamoja katika mkutano wa G20.,
    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako