• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Mkutano wa G20 utatumiwa kama fursa ya kuvutia uwekezaji barani Afrika

  (GMT+08:00) 2016-08-28 17:03:33

  Waziri wa mahusiano ya kimataifa na ushirikiano wa Afrika Kusini Maite Nkoana-Mashabane amesema mkutano wa kilele wa kundi la G20 utachukua nafasi muhimu katika kuhimiza na kuimarisha biashara na uwekezaji barani Afrika.

  Bibi Mashabane amesema hayo kabla ya mkutano huo kufanyika tarehe 4 na 5, Septemba mjini Hangzhou, mashariki mwa China. Pia amesema Afrika Kusini ikiwa ni nchi pekee ya Afrika kwenye kundi la G20 itatumia nguvu kutafuta maslahi ya bara la Afrika, na kuendelea kujitahidi kufanya uchumi wa dunia ujumuishe hamu na maslahi ya nchi zinazoendelea.

  Wakati huohuo, rais Macky Sall wa Senegal atakayehudhuria mkutano huo akiwa mwenyekeiti wa Mpango Mpya wa Ushirikiano kwa Maendeleo ya Afrika NEPAD amesema atafanya juhudi za kuvutia uwekezaji kwa nchi za Afrika, kutetea utendaji wa haki na kupambana na ukwepaji wa kodi wakati wa mkutano huo. Pia amesisitiza ulazima wa kuwepo kwa uwekezaji zaidi unaoweza kuchangia maendeleo ya nchi za Afrika.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako