• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Majadiliano yaliyofanyika kabla ya Mkutano wa G20 yapata matokeo mazuri

    (GMT+08:00) 2016-08-29 10:42:55

    Waziri wa fedha wa China Lou Jiwei amesema, raundi kadhaa za majadiliano kuhusu sera ya fedha yaliyofanyika mwaka huu kabla ya Mkutano wa kilele wa G20 yamepata matokeo mengi, ambayo yatawasilishwa kwenye mkutano rasmi utakaofanyika mwezi ujao.

    Bw. Lou amesema, maofisa wa taasisi za fedha na Benki Kuu kutoka nchi wanachama wa G20 wameweka vigezo wa kupima mafanikio ya mageuzi ya kimwundo kwa mara ya kwanza katika historia.

    Watunga sera hao wamependekeza kuhimiza mageuzi ya Benki ya Dunia na Shirika la Fedha la Kimataifa IMF, na kuimarisha ushirikiano wa kiuchumi, na kuhimiza nchi zilizoendelea kutimiza ahadi zao za kutoa fedha kwa nchi zinazoendelelea kwa kuzisaidia kupambana na mabadiliko ya hali hewa.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako