• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Vifaranga vya ndege vinavyolia zaidi vinapata matunzo mazuri zaidi kutoka kwa wazazi wao

    (GMT+08:00) 2016-08-30 15:59:02

    Utafiti kuhusu mawasiliano kati ya ndege wazazi na vifaranga unaonesha kuwa wakati vifaranga vya ndege vinapokuwa na shinikizo, vinatoa milio mikubwa zaidi kuliko kawaida, hivyo wazazi wao wanawatunza kwa makini zaidi.

    Watafiti kutoka idara mbalimbali za utafiti wa sayansi za Ufaransa na Australia wameshirikiana kutafiti vitendo vya ndege wazazi aina ya shorewanda milia baada ya kusikia milio mbalimbali ya watoto wao katika jangwa la jimbo la New South Wales nchini Australia.

    Watafiti waliwapiga baadhi ya vifaranga vya ndege sindano ya homoni inayosababisha shinikizo. Baada ya kulingana na milio ya vifaranga vya ndege kufuatia kupigwa sindano na kabla ya hapo, wamegundua kuwa ndege hao wakiwa na shinikizo, wanatoa milio mikubwa zaidi. Watafiti pia wameweka vyombo vya uchunguzi kwenye miili ya wazazi wao, ili kurekodi vitendo vyao na wakati wa kutoka na kurudi kwenye viota.

    Matokeo yanaonesha kuwa baada ya kusikia milio mikubwa ya watoto wao, si kama tu ndege wazazi wanatafuta chakula kwa bidii zaidi, bali pia wanakaa kwenye viota kwa muda mrefu zaidi ili kutuliza watoto wao. Uzito wa vifaranga vya ndege waliopigwa sindano unaongezeka kwa kasi zaidi kuliko wengine, hii inamaanisha kuwa wamepata matunzo mazuri zaidi kutoka ka wazazi wao.

    Kituo cha utafiti wa sayansi cha Ufaransa kimesema utafiti huo umethibitisha kuwa vifaranga vya ndege vinaweza kuwaambia wazazi wao shinikizo lao, na kuwahimiza wazazi kuwatunza kwa makini zaidi.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako