• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Mkutano wa G20 kutoa uzoefu na fursa kwa nchi zinazoendelea

    (GMT+08:00) 2016-08-30 16:19:28

    Profesa wa Taasisi ya Teknolojia ya IIIionois ya Marekani Khairy Tourk amesema mkutano wa kilele wa kundi la G20 utakaofanyika hivi karibuni mjini Hangzhou utatoa fikra na mwelekeo mpya kwa maendeleo ya dunia na pia kutoa uzoefu na fursa kwa nchi zinazoendelea. Pili Mwinyi anatuelezea zaidi.

    Ripoti iliyotolewa mwezi uliopita na Shirika la Fedha Duniani IMF ilipunguza makadirio ya ukuaji wa uchumi wa dunia kwa mwaka huu na mwaka kesho hadi asilimia 3.1 na asilimia 3.4, viwango ambavyo vyote viko chini ya vile vilivyokadiriwa mwezi Aprili. Profesa Tourk amesema tangu msukosuko wa fedha uibuke mwaka 2008, ambao umeathiri vibaya uchumi wa dunia, sera za fedha zinazotolewa moja baada ya nyingine zinaweza kukuza uchumi ndani ya muda mfupi, lakini zimeshindwa kutoa injini halisi za ukuaji huo kama ilivyotarajiwa na wafanya maamuzi.

    Profesa Tourk anaona kuwa mageuzi ya sekta ya utoaji yanahitajika sana, na dhamira za kisiasa za serikali za nchi mbalimbali zitaamua kama yatafanikiwa au la. Amesema kama wachumi wengine wengi, ana matumaini mazuri na mageuzi ya kiuchumi yanayoendelea nchini China.

    "Mageuzi ya China ni ya pekee yanayovutia watu. Kuibuka kwa China kumeiletea dunia mabadiliko mengi, na pia kuifanya nchi hiyo kuwa nguvu na injini kuu za uchumi wa dunia."

    Profesa Tourk amesema cha kufurahisha ni kwamba maendeleo ya viwanda ya nchi zinazoendelea yamekuwa ajenda muhimu ya kujadiliwa kwenye mkutano wa kilele wa kundi la G20, na aona kuwa maendeleo na mageuzi ya uchumi wa China yatatoa uzoefu na fursa kwa nchi nyingine zinazoendelea, na Benki ya Uwekezaji wa Miundombinu ya Asia AIIB, Mfuko wa Hariri na Benki ya Maendeleo Mapya, mashirika ambayo yameanzishwa katika miaka ya hivi karibuni kutokana na mapendekezo ya China pia yatatoa fedha zinazozihitajika kwa ujenzi wa miundombinu ya nchi zinazoendelea.

    "Ujenzi wa miundombinu unaweza kusaidia nchi nyingi kujenga uchumi wa kisasa, na hili ni lengo ambalo bado halijatimizwa kutokana na miundombinu mibovu. Miundombinu mizuri inaweza kusaidia kuvutia uwekezaji wa kigeni, na kutengeneza nafasi nyingi za ajira."

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako