• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Kamata wizi kwa kutafiti kadi za kupanda mabasi

    (GMT+08:00) 2016-08-31 11:04:11

    Kadi za kupanda mabasi zimerahisisha maisha yetu, hatuna haja ya kubeba pesa nyingi ili kupanda mabasi. Lakini watafiti wamesema kadi hizi huenda zikwa zinasaidia kuthibitisha wizi. Wametafiti data za kadi mjini Beijing, na kuthibitisha karibu asilimia 93 ya wizi kwa mafanikio.

    Prof Xiong Hui na watafiti wengine kutoka Chuo Kikuu cha Rutgers cha Marekani wamesema abiria wengi wanapopanda mabasi au subway, wanachagua njia zinazotumia muda mfupi zaidi au zinazobadili mabasi kwa mara chache zaidi, lakini wachache wanasafiri kwa njia za ajabu, kwa mfano, wanasafiri kwa njia inayozunguka mji au wanabadili mabasi ghafla. Kama mtu fulani siku zote anasafiri kwa njia za ajabu, huenda akawa ni mwizi.

    Watafiti wametafiti data za kadi za kupanda mabasi zilizorekodiwa kati ya Aprili hadi Juni mwaka 2014 mjini Beijing ambazo zinahusu abiria milioni 6 ambao walitumia kadi hizi kwa mara bilioni 1.6, njia 896 na vituo elfu 45 vya mabasi, njia 18 na vituo 320 vya subway.

    Matokeo ya utafiti yanaonesha kuwa ni kweli asilimia 92.7 ya wizi waliokamatwa waliwahi kupanda mabasi kwa njia za ajabu, lakini inaonekana kutafuta wizi kwa data za kadi si njia yenye ufanisi, kwani mmoja kati ya watu 14 waliopanda mabasi kwa njia za ajabu mwishowe alithibitishwa kuwa ni mwizi.

    Prof. Xiong Hui alisema kutafuta wizi kwa kamera ni njia yenye ufanisi zaidi kuliko kutafiti data za mamilioni ya abiria.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako