• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Mkutano ujao wa marais wa China na Marekani unalenga kupunguza pengo na kupanua ushirikiano

    (GMT+08:00) 2016-08-31 18:21:37

    Mkutano unaotarajiwa kufanyika kati ya rais Xi Jinping wa China na rais Barack Obama wa Marekani utalenga kupunguza tofauti na kupanua ushirikiano wa kivitendo kati ya nchi hizo mbili.

    Mkurugenzi wa masuala ya Asia katika baraza la usalama wa taifa la Marekani Daniel Kritenbrink amesema, rais Obama atakuwa na mazungumzo marefu na rais Xi wa China kabla ya mkutano wa G20 utakaoanza mwishoni mwa wiki hii hapa China. Amesema rais Obama ataweka wazi kama alivyofanya siku za nyuma kuwa Marekani inapongeza China inayoibuka ambayo ni ya amani, utulivu, na ustawi, na ni mwenza anayewajibika katika masuala ya kimataifa.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako