• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Rais wa China akutana na mrithi wa mfalme wa Saudi Arabia

    (GMT+08:00) 2016-08-31 21:20:29

    Rais Xi Jinping wa China leo hapa Beijing amekutana na mrithi wa mfalme wa Saudi Arabia Mohammed bin Salman Al Saud.

    Kwenye mazungumzo yao, rais Xi amesema, katika miaka 26 iliyopita tangu China na Saudi Arabia zianzishe uhusiano wa kibalozi, nchi hizo mbili zimetendeana kwa dhati, urafiki, na usawa, na mafanikio mengi ya ushirikiano baina yao yamepatikana katika sekta mbalimbali. Amesema China inaichukulia Saudi Arabia kuwa mwenzi muhimu wa ushirikiano katika kuhimiza mpango wa "Njia Moja na Ukanda Mmoja", na inapenda kufanya juhudi na nchi hiyo kwa pamoja, ili kuwanufaisha zaidi watu wa nchi hizo mbili na kuchangia amani ya kikanda na kote dunia.

    Naye Bw. Mohammed amesema, serikali yake na watu wa nchi yake wanatilia maanani sana uhusiano na China, ambayo ni rafiki muhimu wa kimkakati. Ameongeza kuwa, Saudi Arabia inaunga mkono kithabiti msimamo wa China katika suala la Taiwan na Bahari ya Kusini ya China, na inapenda kuimarisha ushirikiano kati ya nchi hizo mbili katika uchumi, biashara na mambo ya fedha.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako