• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Rais wa Misri asema kaulimbiu ya mkutano wa kilele wa G20 inaonesha kihalisi mahitaji ya maendeleo ya uchumi duniani

    (GMT+08:00) 2016-09-01 15:29:40
    Rais Abdel Fattah al Sisi wa Misri amesema, kaulimbiu ya mkutano wa kilele wa G20 utakaoanza mwishoni mwa wiki hii inaonesha kihalisi mahitaji ya maendeleo ya uchumi duniani.

    Safari hii kwenye mkutano wa G20, washiriki watafanya majadiliano chini ya kaulimbiu ya "Kujenga Uchumi wa Dunia ulio na Uvumbuzi, Uhai, Ushirikiano na Jumuishi". Rais Sisi amesema, msukosuko wa fedha ulioibuka katika baadhi ya nchi unaweza kuenea hadi nchi nyingine na kusababisha uchumi kushuka na shughuli za biashara kupungua, huku kaulimbiu ya mkutano huu wa G20 ikiwa inaonesha kihalisi mahitaji ya maendeleo ya uchumi duniani. Amesema nchi yake itaimarisha ushirikiano na nchi nyingine wanachama wa kundi la G20 na zile zilizojitokeza kiuchumi hivi karibuni, na kutekeleza kwa vitendo mafanikio yatakayopatikana kwenye mkutano huo.

    Aidha rais Sisi ameeleza matumaini yake kuwa, nchi hizo zinatarajiwa kushirikiana kuziba njia za kukusanya fedha na silaha kwa makundi ya kigaidi, ili kuzuia kwa pamoja kuenea kwa ugaidi duniani.
    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako