• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Marekani yatoa mwito wa kutumia mkutano wa G20 kuhimiza ongezeko jumuishi

    (GMT+08:00) 2016-09-01 15:30:01
    Waziri wa fedha wa Marekani Jacob Lew ametoa wito wa kutumia sera na hatua mbalimbali zikiwemo zile za kifedha ili kutimiza ongezeko jumuishi.

    Amesema, G20, likiwa ni jukwaa muhimu kwa viongozi wa nchi zake wanachama kujenga hali ya kuaminiana miongoni mwao, linafanya kazi kubwa katika kuhimiza ukuaji wa uchumi na utulivu wa fedha. Bw. Jacob pia amesema, kwenye hotuba yake atakayotoa katika mkutano wa kilele wa G20 utakaofanyika Hangzhou, rais Barack Obama atatoa mwito wa kutilia maanani ongezeko jumuishi na kutunga sera zinazolenga kuongeza nafasi kwa vijana na wanyonge.

    Ameongeza kuwa G20 inatoa mchango mkubwa katika kukabiliana na mabadiliko ya tabianchi na changamoto nyingine za kimazingira kwa kuanzisha kikundi kipya cha utafiti wa mambo ya fedha yasiyochafua mazingira.
    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako