• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Mwanasayansi alipocheza na mtoto wake aligundua njia mpya ya kuinua uwezo wa darubini kwa utando wa buibui

    (GMT+08:00) 2016-09-01 16:23:30

    Utafiti mpya ulioripotiwa na gazeti la Nano Letters la Marekani unaonesha kuwa utando wa buibui ni malighafi nzuri ya kimaumbile ya kutengeneza darubini, na inaweza kutumiwa kuinua uwezo wa darubini za jadi za kuangalia vitu vidogovidogo viilivyotengenezwa kwa vioo.

    Utafiti huo uliongozwa na Dr. Wang Zengbo kutoka Chuo Kikuu cha Bangor cha Uingereza na kushirikiwa na Prof. Fritz Vollrath kutoka Chuo Kikuu cha Oxford.

    Kutengeneza darubini kwa utando wa buibui ni rahisi sana. Watafiti waliweka utando wa buibui juu ya kitu kitakachoangaliwa, kutia kileo katika kitu hiki na utando wa buibui, halafu kuangalia kitu hiki kupitia darubini ya kawaida ya vioo. Utando wa buibui unainua uwezo wa darubini ya vioo kwa mara mbili hadi tatu, na kuwawezesha kuona vitu vidogovidogo vyenye urefu wa nanomita 100 tu. Wakitumia darubini ya vioo tu hawawezi kuona.

    Dr. Wang alisema aligundua jambo hili kwa bahati. Siku moja alipocheza na mtoto wake katika ua wa nyumba yake aliona utando wa buibui. Ghafla akapata wazo la kutengeneza darubini kwa utando huo, baadaye alithibitisha kuwa wazo hili kweli linafanya kazi.

    Dr. Wang alisema huenda kuna malighafi nyingine zinazofanya kazi vizuri zaidi kuliko utando wa buibui katika mazingira ya kimaumbile, na wataendelea kufanya juhudi ya kutafuta malighafi hizi.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako