• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • China itaonesha sura ya kuwa nchi kubwa inayowajibika katika mkutano wa G20

    (GMT+08:00) 2016-09-01 19:37:29

    Ikiwa zimebaki siku 3 kabla ya kufanyika kwa mkutano wa kilele wa G20, viongozi wa nchi wanachama wa kundi hili, nchi washiriki zilizoalikwa, pamoja na wakuu wa mashirika makuu 7 ya kimataifa watafika katika mji wa Hangzhou, unaojulikana kwa jina la "pepo ya duniani" ili kujadili ajenda zinazohusu uchumi na usimamizi duniani. Pili Mwinyi anatuelezea zaidi.

    Mtaalamu wa uchumi wa kimataifa wa Shanghai Zhang Haibing anaona kuwa kuandaa mkutano wa kilele wa G20 kunaonesha kuongezeka kwa ushawishi wa China kwenye jumuiya ya kimataifa.

    "Kundi la G20 linalenga zaidi kushughulikia usimamizi wa uchumi duniani, lakini unaweza kuona mada kuhusiana na mzingira, usalama, maendeleo ya kijamii na hata afya pia zinajadiliwa katika kundi hilo, hali hii ambayo ni changamoto kwa nchi moja katika sekta ya diplomasia, hivyo mkutano wa kilele wa G20 wa safari hii ni matokeo ya juhudi tulizofanya na pia ni uthibitisho wa nguvu za China."

    Katika siku kadhaa zijazo, rais Xi Jinping wa China atahudhuria mikutano mbalimbali, ambapo ataitumia kujadiliana na viongozi wa nchi washiriki kuhusu ajenda muhimu, na pia kueleza misimamo ya China. Mwanadiplomasia mwenye uzoefu wa China Wang Yusheng anasema

    "Ikiwa mwenyeji wa mkutano wa kilele wa G20, China itatumia fursa hii kuonesha sura yake ya kuwajibika na kuunganisha busara za China na za nchi nyingine. Sisi tunasisitiza usawa na kusaidiana, mtazamo sahihi kuhusu maslahi, mashauriano na kunufaika kwa pamoja mafanikio na pia jumuiya yenye hatma ya pamoja, na China itaeneza mawazo hayo na kufanya ushirikiano katika kukabiliana na changamoto mbalimbali."

    Wakati wa mkutano huo, rais wa China pia atakutana na kufanya mazungumzo ya pande mbili na wenzake wa nchi mbalimbali, ambapo mkutano kati yake na rais Barack Obama wa Marekani unafuatiliwa zaidi. Profesa wa Chuo Kikuu cha Umma cha China, kitivo cha uhusiano wa kimataifa Wang Yiwei anasema

    "Hii ni mara ya mwisho kwa Obama kutembelea China akiwa rais wa Marekani. Naona katika ziara hiyo, ataeleza mambo mengi yanayohitaji kufanyiwa ushirikiano kati ya China na Marekani."

    Wakati huohuo, rais wa China pia atakutana na mwenzake wa Russia Vladimir Putin miezi miwili tu baada ya mazungumzo yao yaliyopita.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako