• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Manchester City yamtetea Sergio Aguero kwa kudaiwa kumpiga kiwiko Winston Reid

    (GMT+08:00) 2016-09-02 08:35:52

    Klabu ya Manchester City ya Uingereza jana ilimtetea mshambuliaji wake wa kimataifa wa Argentina Sergio Aguero baada ya kudaiwa kumpiga kiwiko kwa makusudi Winston Reid wa West Ham United wakati wa mchezo dhidi yao. Man City inamtetea Aguero ili kumuokoa na adhabu ya kufungiwa mechi tatu, endapo chama cha soka cha Uingereza FA kitamkuta na hatia ya kosa la kumpiga kiwiko kwa makusudi Winston Reid.

    Sergio Aguero ambaye anakosekana katika kikosi cha timu ya taifa ya Argentina kitakachocheza michezo ya kuwania kufuzu Kombe la Dunia, kama akikutwa na hatia atakosa mchezo dhidi ya wapinzania\ wao Man United September 10, mchezo wa EFL Cup dhidi ya Swansea City na mchezo wa EPL dhidi ya AFC Bournemouth.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako