• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Benki ya Maendeleo Mapya ya BRICS yatarajia mkutano wa G20 utaongoza ushirikiano unaoleta maendeleo endelevu duniani

    (GMT+08:00) 2016-09-02 15:15:23

    Naibu mkuu wa Benki ya Maendeleo Mapya ya BRICS Bw. Paulo Nogueira Batista amesema, mkutano wa kilele wa G20 utakaoanza kesho mjini Hangzhou, China, utatoa fursa kwa Benki hiyo iliyoanzishwa mwaka jana kushiriki kwenye usimamizi wa dunia na kujitokeza kwenye jukwaa la kimataifa.

    Amesema China inatumia fursa ya kuwa mwenyeji wa mkutano huo kutoa wito kwa nchi mbalimbali kujadili utekelezaji wa ajenda ya maendeleo endelevu ya mwaka 2030, na ajenda kuhusu mambo ya fedha yasiyochafua mazingira itajadiliwa kwa mara ya kwanza kwenye mkutano huu.

    Ameongeza kuwa katika miaka mitano ijayo Benki ya Maendeleo Mapya ya BRICS itaupa kipaumbele mpango wa miundombinu endelevu, kama vile usimamizi wa maliasili endelevu na maji.
    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako