• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Matukio makubwa yaliyotokea wiki hii ( Agusti 27-Septemba 2)

  (GMT+08:00) 2016-09-02 18:54:21

  Rais wa Gabon Ali Bongo ametangazwa mshindi wa Uchaguzi wa urais

  Rais wa Gabon Ali Bongo ametangazwa mshindi wa Uchaguzi wa urais uliofanyika mwishoni mwa wiki iliyopita.

  Waziri wa Mambo ya ndani wa nchi hiyo Pacome Moubelet-Boubeya Jumatano jioni alitangaza matokeo hayo ya mwisho na kubainisha kuwa rais Bongo alikuwa ameibuka mshinidi kwa kupata asilimia 49.80 ya kura dhidi ya mpinzani wake wa karibu Jean Ping aliyepata asilimia 48.23

  Lakini pindi tu baada ya kutangazwa kwa matokeo hayo, kumekuwa na maandamano na fujo kutoka kwa upande wa upinzani unaodai kwamba kura ziliibiwa.

  Waandamanaji wenye hasira nchini humo Gabon walichoma moto bunge la nchi hiyo wakipinga ushindi wa Bongo.

  Serikali nchini Gabon imewakamata zaidi ya watu elfu moja katika siku ya pili ya ghasia zilizozushwa na wapinzani waliokuwa wakipinga matokeo ya uchaguzi wa Rais uliofanyika nchini humo Jumamosi iliyopita.

  Ripoti kutoka katika mji mkuu wa Gabon Libreville, zinasema kuwa watu watatu wameuawa katika ghasia hizo.


  1 2 3 4 5 6 7 8 9
  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako