• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Matukio makubwa yaliyotokea wiki hii ( Agusti 27-Septemba 2)

    (GMT+08:00) 2016-09-02 18:54:21

    Maandamano yaendelea Zimbabwe dhidi ya serikali

    Nchini Zimbabwe, mvutano unaendelea kushuhudiwa wakati ambapo vyama vya kiraia vimewataka wananchi wa Zimbabwe kubakia nyumbani katika maandamano dhidi ya serikali ya Rais Robert Mugabe.

    Ni miezi kadhaa sasa maandamnao yakiendelea kushuhudiwa nchini humo.

    Wote wanadai kujiuzulu kwa Robert Mugabe, ambaye yuko madarakani kwa miaka 36 sasa, na wanamshtumu kwamba anahusika kwa kuanguka kwa uchumi wa nchi. Kiwango cha ukosefu wa ajira kinakadiriwa kuwa zaidi ya 80% na nchi, hata hivyo, nchini sarafu za kitaifa na inakabiliwa na mfumuko wa bei.

    Serikali ya Zimbabwe imepiga marufuku maandamano kwa wiki mbili mjini Harare kwa lengo la kuzuia vurugu.

    Kwa mujibu wa Radio ya taifa ya Zimbabwe amri hiyo inatekelezwa kuanzia tarehe 1 hadi 16 Septemba.

    Amri hiyo inakuja kabla ya maandamano ya vyama vya upinzani yaliyopangwa kufanyika leo ambayo yanalenga kuilazimisha serikali kutekeleza mabadiliko ya sheria ya uchaguzi kabla ya uchaguzi ujao utakaofanyika mwaka 2018.


    1 2 3 4 5 6 7 8 9
    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako