• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Matukio makubwa yaliyotokea wiki hii ( Agusti 27-Septemba 2)

    (GMT+08:00) 2016-09-02 18:54:21

    Waziri wa zamani ahukumiwa Malawi

    Mahakama Kuu mjini Lilongwe, nchini Malawi wiki hii, imewmuhukumu Waziri wa zamani wa sheria, Raphael Kasambara, kifungo cha miaka 13 jela na kuamurishwa kufanya kazi ngumu kwa kosa la kula njama ya mauaji.

    Bw Kasambara amepatikana na hatia ya kula njama katika mauaji mwezi Septemba 2013 ya mkurugenzi wa zamani wa Bajeti katika Wizara ya Fedha, Paul Mphwiyo.

    Mauaji ya Bw Mphwiyo yalipelekea ugunduzi wa kashfa ya uporaji wa rasilimali za umma wakati wa utawala wa Rais Joyce Banda, kashfa ambayo ilibatizwa jina la "cashgate".

    Karibu milioni 250 zililipwa kwa udanganyifu kwa wafanyabiashara kwa ajili ya huduma ambazo hazikuwahi kufanyika.

    Siku chache kabla ya kashafa hiyo, afisa mkuu wa serikali alikutwa na dhahabu nyingi zinazomilikiwa na mamlaka ya Hazina ya Serikali, sawa na zaidi ya dola za Marekani milioni 300, ndani gari lake.

    Fedha hizo pia zilihifadhiwa ya magari nyumbani kwa baadhi ya maafisa wa serikali.

    Mara tu baada ya hukumu dhidi yake mwezi uliopita, Kasambara aliarifu kuwa kamwe hatakata rufaa wa uamuzi wa Mahakama.


    1 2 3 4 5 6 7 8 9
    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako