• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Matukio makubwa yaliyotokea wiki hii ( Agusti 27-Septemba 2)

    (GMT+08:00) 2016-09-02 18:54:21

    Wavenezuela waandamana kupinga utawala

    Maelfu ya watu nchini Venezuela wameshiriki maandamano ya upinzani katika mji mkuu wa Caracas wakitaka kuondolewa madarakani kwa Rais Nicolas Maduro.

    Wanadai kwamba hawataiacha haki yao ya kikatiba kuandamana kwa amani mpaka pale kutakapokuwa na uchaguzi wa amani, wa kidemokrasia wa mabadiliko ya katiba.

    Wanamlaumu Rais Nicolas Maduro kuhusiana na uchumi mbaya wa nchi hiyo na kuituhumu pia Tume ya Taifa ya nchi hiyo kwa makusudi kuchelewesha kura ya maoni ambayo ingeweza kufupisha uwepo wake madarakani.

    Hata hivyo wafuasi wa Rais Maduro, ambao chama cha Kisoshalisti kimetawala nchi hiyo kwa miaka 17, pia waliandamana kwa idadi kubwa.

    Kabla ya kuanza kwa maandamano hayo wanasiasa kadhaa wa upinzani walikamatwa.


    1 2 3 4 5 6 7 8 9
    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako