• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Matukio makubwa yaliyotokea wiki hii ( Agusti 27-Septemba 2)

    (GMT+08:00) 2016-09-02 18:54:21

    Rousseff aondolewa madarakani

    Baraza la juu la bunge la Brazil limepitisha mswada wa kumwengua rais Dilma Rousseff kwa kura 61 za ndiyo na dhidi ya 20 za hapana.

    Hii inamaanisha kuwa Dilma Rousseff, rais wa kike wa kwanza katika historia ya Brazil amevuliwa wadhifa huo na haruhusiwi kushika wadhifa wowote katika serikali ndani ya miaka minane, na nafasi yake imechukuliwa na Michel Temer ambaye alikuwa makamu wake.

    Baada kuapishwa, Bw. Michel Temer kutoka chama cha PMDB ambaye atakuwa madarakani mpaka mwaka 2018, amesema ataiokoa nchi hiyo kutoka mgogoro wa kiuchumi na kisiasa.

    Rousseff ameshitakiwa kwa kutaka kuficha mapungufu ya bajeti ya umma kwa kupitia utaratibu wa fedha, ikiwemo kuchelewesha malipo ya mikopo kwa benki, na kuagiza mikopo zaidi bila kupitishwa na bunge.


    1 2 3 4 5 6 7 8 9
    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako