• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Matukio makubwa yaliyotokea wiki hii ( Agusti 27-Septemba 2)

    (GMT+08:00) 2016-09-02 18:54:21

    Trump azuru Mexico.

    Mgombea Urais wa Marekani kwa chama cha Republican Donald Trump wiki hii amefanya ziara nchini Mexico kukutana na Rais wa nchi hiyo Enrique Pena Nieto masaa machache tu kabla ya kutangaza sera yake kuhusu uhamiaji.

    Amesema kwa njia ya Twitter kwamba anakubali mwaliko wa rais Pena Nieto na kwamba watafanya kikao cha faragha.

    Pindi tu baada ya mkutano huo kwenye hotuba yake kuhusu sera ya Uhamiaji, Trump alisistiza kwamba Marekani itajenga ukuta kuzuia uhamiaji ikiwa atachaguliwa kuwa rais.

    Alisema Mexico itagharamia kujengwa kuwa ukuta huo, lakini naye rais Nieto alisema amemwambia wazi kwamba nchi yake kamwe haitagharamia.

    Trump amekuwa akishikilia msimamo kwamba atajenga ukuta kati ya mpaka wa Marekani na Mexico kuzuia wahamiaji kuingia nchini humo na kwenye kampeni zake za awali amewataja wamexico kama "wezi na wabakaji."


    1 2 3 4 5 6 7 8 9
    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako