• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • IMF yatoa wito wa kuchukua hatua ili kuepukana na mtego wa kiwango cha chini cha ongezeko la uchumi wa dunia

    (GMT+08:00) 2016-09-02 20:36:46

    Shirika la Fedha la Kimataifa(IMF) limetoa ripoti likitoa wito kwa nchi mbalimbali wanachama wa kundi la G20 kuchukua hatua madhubuti za kuhimiza ongezeko endelevu, jumuishi na lenye nguvu la uchumi.

    Ripoti hiyo imesema, ongezeko la uchumi wa dunia litaendelea kukosa nguvu katika siku za baadaye, na nchi wanachama wa kundi la G20 zinatakiwa kuimarisha mageuzi ya muundo wa uchumi, kuongeza matumizi ya sera za fedha na sarafu na ushirikiano kati yao ili kuendelea kusukumba mbele utandawazi, kulinda hadhi ya biashara katika kuhimiza ongezeko la uchumi, kupunguza gharama vikwazo vya biashara.

    Mkurugenzi wa Shirika la Fedha la Kimataifa IMF Bi. Christine Lagarde amesema, kwenye mkutano wa kilele wa kundi la G20 utakaofanyika huko Hangzhou, China, viongozi wa nchi za kundi hilo watajadili mada muhimu mfululizo, zikiwemo ongezeko dhaifu la uchumi, ukosefu wa usawa, na kuendelea taratibu kwa mageuzi ya muundo wa uchumi.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako