• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Vyombo vya habari vya Afrika vyafuatilia mkutano wa G20

    (GMT+08:00) 2016-09-02 20:37:34

    Wakati mkutano wa kilele wa G20 ukitarajiwa kuanza wikiendi hii mjini Hangzhou, mashariki mwa China, China imetoa pendekezo la kufanya ushirikiano na nchi za Afrika na zile zilizo nyuma kimaendeleo ili kuhimiza maendeleo ya kiviwanda huku waziri wa mambo ya nje wa China Wang Yi akisema, China inapenda kushirikiana na nchi nyingine wanachama wa kundi la G20 kupata mafanikio kumi kwenye mkutano huo, na moja kati yao yanahusu Afrika. Hivi sasa vyombo vya habari duniani vikiwemo vile vya nchi za Afrika vimeelekeza ufuatiliaji wao mjini Hangzhou. Pili Mwinyi anatuelezea zaidi.

    Redio ya SIBUKA nchini Tanzania imesema kaulimbiu ya mkutano huo ni "Kujenga Uchumi wa Dunia ulio wa Uvumbuzi, Uhai, Ushirikiano na Ujumuishi". Na katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa Bw. Ban Ki-moon ameipongeza China kwa kuandaa mkutano huo, akisema wazo la maendeleo endelevu litasisitizwa katika mchakato mzima wa mkutano huo, hii ndio inayohitajika duniani.

    Redio ya biashara nchini Bostwana Duma imesema Afrika Kusini ni nchi pekee mwanachama wa kundi la G20 kutoka Afrika, lakini mkakati wa kimaendeleo na mitaji mingi iliyotolewa na China katika miaka ya hivi karibuni barani Afrika vimewezesha serikali ya nchi za Afrika na watu wake kupenda kuamini kuwa China inaweza kufanya ushirikiano mzuri na Afrika. Pia imesema mbali na Afrika Kusini, nchi nyingine mbili za Afrika za Misri na Senegal pia zimealikwa kushiriki katika mkutano huo, kwa hivyo Botswana inafuatilia sana mkutano huo na kutarajia nchi za Afrika ziweza kupata manufaa.

    Kabla ya kuelekea Hangzhou kuhudhuria mkutano wa kilele wa G20, rais Macky Sall wa Senegal alipohojiwa na vyombo vya habari alisema kundi la G20 linaundwa na nchi zilizoendelea na zile zilizoibuka hivi karibuni kiuchumi, na inatazamiwa kuwa mkutano wa kilele wa Hangzhou utachangia uchumi wa dunia haswa maendeleo ya uchumi wa Afrika.

    Hivi karibuni, Wizara ya Mambo ya Nje ya China imesema nchi nyingi zenye nguvu kubwa za kiuchumi zitakutana kwenye mkutano wa kilele wa G20 wa safari hii, na hii itatoa fursa nzuri za kimaendeleo kwa nchi zinazoendelea, na China ikiwa nchi kubwa zaidi inayoendelea kwenye mkutano huo, ina wajibu wa kuzitafutia manufaa nchi mbalimbali zinazoendelea duniani.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako