• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Rais Xi Jinping wa China akutana na viongozi wa nchi za Afrika

    (GMT+08:00) 2016-09-03 20:02:14

    Rais Xi Jinping wa China amekutana kwa nyakati tofauti na rais Idriss Deby wa Chad ambaye ni mwenyekiti wa zamu wa Umoja wa Afrika na rais Jacob Zuma wa Afrika Kusini ambao wako ziarani nchini China kuhudhuria mkutano wa kilele wa kundi la G20.

    Alipokutana na rais Deby, rais Xi amemkaribisha kuhudhuria mkutano huo kwa niaba ya Umoja wa Afrika na kusema China inaunga mkono Afrika ishiriki kwenye usimamizi wa dunia na kutoa mchango kwa ajili ya kuhimiza ukuaji wa uchumi wa dunia.

    Kwa upande wake rais Deby ameishukuru China kuialika Chad kuhudhuria mkutano huo kwa niaba ya Umoja wa Afrika, na pia ameishukuru China kwa juhudi zake za siku zote za kuisaidia Afrika na kuimarisha ushirkiano wa kunufaishana na Afrika, na vilevile kuongoza kundi la G20 kutilia maanani maendeleo ya Afrika.

    Rais Xi akikutana na rais Zuma wa Afrika kusini amesema, China inapenda kushirikiana na Afrika Kusini kuhimiza uhusiano kati ya nchi hizo mbili ufikie kwenye ngazi mpya. Amesema China na Afrika Kusini zitapanua uaminifu wa kisiasa, kuimarisha mawasiliano kati ya vyama vya kisiasa, serikali, mabunge na majeshi, ili kimarisha ushirikiano wa kimkakati.

    Kwa upande wake rais Zuma amesema, Afrika Kusini na China zimejenga urafiki tangu enzi na dahari, na Afrika Kusini inathamini uhusiano wa wenzi wa kimkakati kati ya pande hizo mbili. Amesema uhusiano kati ya nchi hizo mbili unaimarika siku hadi siku, huku ushirikiano wa sekta mbalimbali ukiendelezwa haraka.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako