• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Viongozi mahiri wamininika Hangzhou

    (GMT+08:00) 2016-09-04 17:56:45
    Mkutano wa kilele wa G20 unaendeela mjini Hangzhou, mashariki mwa China.

    Viongozi wanawacha wa nchi za G20, wanahabari, wakuu wa mashikra makubwa ya kiuchumi na kifedha kama vile benki ya dunia na IMF wanashiriki kwenye mkutano huo.

    Siku ya Jumamosi tarehe 03 Septemba jiji la Hanghzhou liligeuka na kuwa kitovu cha Dunia baada ya kupokea idadi kubwa ya viongozi wanaounda ushirika wa kiuchumi wa G20.

    Katibu Mkuu wa Shirikisho la Uchumi na Maendeleo (OECD) Bw. Angel Gurria akizungumzia kwa ufupi historia ya OECD alisema mnamo Disemba 14 1960, mataifa 20 yalisaini makubaliano ya kuunda umoja huo ambao kwa sasa una jumla ya wanachama, 15 yenye ushawishi mkubwa katika uchumi duniani.

    Bw. Gurria alisema malengo mahsusi ya mkutano huu unaoendelea ni kuzuia mgogoro unaoweza kusababishwa na mataifa au taifa moja kuuza bidhaa nyingi kwa mpigo katika mataifa fulani na kuwanyima wengine haki hiyo.

    Pia anaongeza kwamba hata haki ya kuagiza malighafi haitakiwi kufanywa kwa siri na akafafanua kwamba taifa linaweza kuitwa limeendelea kutokana na kufanya biashara zinazozingatia maadili, na pia kupima pato la ndani la taifa hilo na uzalishaji wake kwa ujumla (GDP).

    Aidha alisema kwamba lengo ni kuzingatiwa kwa makubaliano kadhaa kama yalivyofikiwa na shirikisho la kimataifa la biashara WTO ili kuzuia rushwa, na mikataba mibovu. Lakini pia ni kujenga utamaduni wa uwazi katika miktaba mbali mbali na suala zima la ulipaji wa kodi.

    Katika hotuba yake Rais wa China Xi Jinping ambaye ndiye mwenyeji alisema kwamba biashara kwenye ngazi za kimataifa zinatakiwa kuzingatia usawa na kuhakikisha kwamba mataifa madogo hayaumizwi na mfumo uliopo.

    Waziri Mkuu wa Australia Bw. Malcom Turnbull alisisitiza juu ya ushirikiano ili kukabiliana na uhamishaji haramu wa pesa na ukwepaji wa kodi wa makampuni makubwa ya kimataifa.

    Lakini Rais wa Benki ya Dunia Jim Yong Kim alisistiza kwamba uchumi wa Dunia unatakiwa uwe shirikishi na uzingatie usawa. Na pia akasema ugaidi duniani limekuwa tatizo kubwa kwa sababu kuna watu wenye nguvu wanayafadhili makundi ya kigaidi.

    Zaidi ya hayo alizungumzia juu ya uwekezaji katika miundombinu, na ushirikiano katika kuondoa umaskini na kukabiliana na chanagamoto za Tabia Nchi. Alisifia juu ya lindi la ubunifu linalofanywa na wenyeji Serikali ya China.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako