• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Mkutano wa kilele wa G20 wafunguliwa Hangzhou, China

    (GMT+08:00) 2016-09-04 18:44:30

    Mkutano wa kilele wa kundi la nchi 20 umefunguliwa rasmi leo alasiri mjini Hangzhou, China. Rais Xi Jinping wa China ambayo ni nchi mwenyekiti wa G20, amehutubia ufunguzi wa mkutano huo ambao ni mara ya kwanza kufanyika nchini China.

    Akitoa hotuba kwenye ufunguzi wa mkutano wa kilele wa G20, Rais Xi Jinping wa China amesema anatarajia nchi washiriki wa mkutano huo zitakusanya busara na kuhimiza ushirikiano, ili kuufanya mkutano huo uweze kutimiza lengo la kuchochea ukuaji wa uchumi wa dunia, kuimarisha ushirikiano wa kiuchumi wa kimataifa na kusukuma mbele maendeleo ya kundi la G20.

    Miaka 8 iliyopita, wakati dunia ilipokumbwa na msukosuko mkubwa wa kifedha, kundi la G20 lilichukua jukumu na kufanikiwa kuurejesha uchumi wa dunia uliodidimia kwenye njia ya utulivu na ufufukaji. Baada ya miaka 8, uchumi wa dunia unaokabiliwa na changamoto mbalimbali umefika tena kwenye hatua muhimu. Kwenye hotuba yake rais Xi Jinping wa China amesema,

    "Mapinduzi mapya ya kiteknolojia na kiviwanda bado hayajapevuka, nchi na makundi yenye uchumi mkubwa zimeanza kuingia kwenye kipindi cha jamii yenye wazee wengi, utandawazi wa uchumi duniani unakumbwa na vizuizi, sera za kujilinda kibiashara zimeanza kutekelezwa, utaratibu wa biashara kati ya pande nyingi umekabiliwa na changamoto, na hatari za kifedha bado zinaongezeka ingawa maendeleo dhahiri yamepatikana katika mageuzi ya usimamizi wa kifedha duniani. katika hali hii, ingawa uchumi wa dunia umedumisha mweleko wa ufufukaji, lakini bado unakabiliwa na changamoto nyingi zikiwemo upungufu wa msukumo, kushuka kwa mahitaji, kuyumbayumba kwa soko la kifedha na kudidimia kwa biashara na uwekezaji wa kimataifa."

    Akizungumzia namna ya kukabiliana na changamoto hizo na kutoa ufumbuzi jumuishi unaoweza kuondoa matatizo yote kwa uchumi wa dunia, rais Xi Jinping ametoa mapendekezo matano.

    "Tunapaswa kuimarisha uratibu wa sera za uchumi, kuhimiza kwa njia mwafaka ukuaji wa uchumi wa dunia na kudumisha utulivu wa kifedha; Tunapaswa kufanya uvumbuzi kwa njia ya kutimiza maendeleo, na kutafuta motisha ya kuchochea ukuaji; Tunapaswa kukamilisha usimamizi wa uchumi wa dunia na kuimarisha uhakikisho wa kimfumo; Tunapaswa kujenga uchumi wa dunia ulio wazi, na kuendelea kuhimiza biashara na uwekezaji huria; na vilevile tunapaswa kutekeleza ajenda ya maendeleo endelevu ya mwaka 2030 na kuhimiza maendeleo shirikishi."

    Kuhusu mustakbali wa maendeleo ya kundi la G20, rais Xi amesema, kundi la G20 linapaswa kufuata mahitaji ya uchumi wa dunia, na kujigeuza kutoka utaratibu wa kukabiliana na msukosuko hadi mfumo wa usimamizi wa muda mrefu. Amesisitiza kuwa G20 inapaswa kukusanya busara na kusikiliza maoni ya pande mbalimbali haswa nchi zinazoendelea, ili kuifanya G20 iwe shirikishi zaidi na kuweza kukidhi vizuri mahitaji ya watu wa nchi mbalimbali.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako