• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Mkutano wa kilele wa G20 kusaidia kuharakisha maendeleo ya viwanda Afrika

    (GMT+08:00) 2016-09-04 20:24:13

    Mkutano wa 11 wa kilele wa kundi la G20 umefunguliwa leo huko Hangzhou, China, ambao umeshirikisha nchi nyingi zaidi zinazoendelea katika historia ya kundi la G20. Mkutano huo kwa mara ya kwanza umetoa kipaumbele kwa suala la maendeleo kwenye mfumo wa sera za dunia nzima, huku ukitoa pendekezo la ushirikiano linalolenga kuunga mkono maendeleo ya viwanda wa Afrika na nchi zilizo nyumba kimaendeleo duniani. Wachambuzi wanaona kuwa China kuweka ajenda hiyo kwenye mkutano huo na kuwaalika nchi za Afrika kuhudhuria mkutano huo kumeonesha kuwa China inazingatia suala la maendeleo la nchi za Afrika.

    Imefahamika kwamba, licha ya nchi wanachama ya Afrika Kusini, nchi tatu za Afrika ambazo ni pamoja na nchi mwenyekiti wa Umoja wa Afrika Chad, nchi mwenyekiti wa Shirika la Mpango wa ushirikiano mpya kwa ajili ya maendeleo ya Afrika NEPAD Senegal na Misri pia zimealikwa kwenye mkutano huo. Rais Macky Sall wa Senegal amesema, Afrika inatafuta ushirikiano wala sio msaada, hivyo inataka kufanya juhudi pamoja na nchi nyingine kutimiza ushirikiano wa kunufaishana, na mkutano wa kilele wa G20 umeleta jukwaa zuri kwa ajili ya lengo hilo.

    "G20 imejumuisha nchi muhimu 20 za kiuchumi duniani, mkutano wa kilele wa G20 na mikutano husika itasaidia maendeleo ya dunia katika usimamizi wa kifedha wa kimataifa na mahusiano ya kibiashara ya kimataifa. Ajenda za mkutano wa G20 pia ni muhimu kwa Afrika, kwa mfano ongezeko la uchumi kutokana na uvumbuzi wa sayansi na teknolojia na uwekezaji. Afrika inahitaji uwekezaji na wenzi wa ushirikiano. Mtazamo mpya wa waafrika ni kubadilisha njia ya msaada kutoka nje, kwa sababu msaada wenyewe hauwezi kuendeleza nchi moja, na bara la Afrika haliwezi kuendelezwa kupitia msaada. Tunahitaji wenzi wa ushirikiano wenye maslahi ya pamoja"

    Mtafiti wa ngazi ya juu wa taasisi ya utafiti wa nchi za BRICS ya chuo kikuu cha Fudan, China Bw. Zhu Jiejin amesema, tangu mwanzo wa karne ya 21, Afrika imekuwa moja ya sehemu za dunia zenye ukuaji wa kasi zaidi wa uchumi, lakini chanzo kimoja cha maendeleo ya Afrika yaliyoko nyuma ni kwamba bara hilo liko katika ngazi ya chini kwenye muundo wa biashara duniani. Kwa mujibu wa takwimu husika, hivi sasa muundo wa biashara na nje wa zaidi ya theluthi mbili za nchi za Afrika bado unabaki uleule wa kipindi cha mwanzo tangu zijipatie uhuru, ambao unategemea bidhaa za msingi za aina moja au mbili za kilimo na madini. Ili kuondoa tatizo hilo, maendeleo ya viwanda yana umuhimu mkubwa kwa Afrika. Pendekezo la ushirikiano lililotolewa kwenye mkutano huu wa G20 la kuunga mkono maendeleo ya viwanda katika Afrika na nchi zilizo nyuma kimaendeleo, limekidhi kwa kiasi kikubwa mahitaji ya Afrika.

    "Lengo la 9 la ajenda ya malengo ya maendeleo endelevu ya mwaka 2030 pamoja na mpango wa kwanza wa maendeleo ya miaka kumi wa ajenda ya mwaka 2063 ya Afrika, halafu tuangalie Pendekezo la ushirikiano lililotolewa kwenye mkutano huu wa G20 la kuunga mkono maendeleo ya viwanda katika Afrika na nchi zilizo nyuma kimaendeleo, tutaona hizi tatu zote zinalingana. Hivyo  tuseme pendekezo lililotolewa kwenye mkutano huo limekidhi kwa kiasi kikubwa ufuatiliaji wa Afrika."

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako