• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Diplomasia ya kiuchumi ya Kenya ina faida kubwa

    (GMT+08:00) 2016-09-05 09:19:30

    Mkurugenzi mtendaji wa jopo la washauri wa Afrika Peter Kagwanja amesema, diplomasia ya uchumi ambayo Kenya inaitumia katika uhusiano wake na nchi nyingine za Afrika na nchi zenye nguvu imeanza kuzaa matunda.

    Katika makala yake iliyochapishwa kwenye gazeti moja la Kenya, Kagwanja amesema hadhi ya Kenya kama kituo cha biashara, uwekezaji, uchukuzi, na ugavi katika kanda hiyo imeimarika kutokana na diplomasia hiyo. Amesema serikali ya Kenya imebadili sera yake ya kigeni ili kuimarisha ushawishi wa nchi hiyo kijeshi, uchumi, diplomasia, na utamaduni.

    Ameongeza kuwa, diplomasia ya uchumi ya Kenya sio tu imeimarisha biashara ya pande mbili na nchi zinazoibuka kiuchumi kama China, lakini pia imevutia mitaji na ujuzi wa kiufundi kutoka nchi nyingine.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako